#Football #Sports

WACHEZAJI WATATU WA AFRIKA KUSINI WATEULIWA KWA TUZO

Mshambulizi wa Nigeria Ademola Lookman na mlinda mlango wa Afrika Kusini Ronwen Williams walikuwa miongoni mwa nyota watano walioteuliwa Jumatatu kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika wa Mwaka.

Taarifa ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) imewataja beki wa Morocco, Achraf Hakimi, winga wa Ivory Coast, Simon Adingra na mshambuliaji wa Guinea, Serhou Guirassy kuwa miongoni mwa wagombea wengine.

Lookman alifunga hat-trick kwa Atalanta katika ushindi wa 3-0 wa fainali ya UEFA Europa League dhidi ya Bayer Leverkusen msimu uliopita na anapendekezwa kushinda tuzo hiyo.

Sherehe ambapo tuzo katika vipengele mbalimbali zitatolewa kwa mastaa wa kiume na wa kike barani Afrika itafanyika katika jiji la Marrakesh nchini Morocco mnamo Desemba 16.

Imetayarishwa na Nelson Andati

WACHEZAJI WATATU WA AFRIKA KUSINI WATEULIWA KWA TUZO

NZOIA SUGAR YALAMBA SUKARI YA USHINDI

WACHEZAJI WATATU WA AFRIKA KUSINI WATEULIWA KWA TUZO

KANE ASISITIZA MSISIMUKO KWA KIKOSI CHAKE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *