WAHALIFU WAKULIMA

Utunzaji wa wanyamapori umewawezesha Vijana waliokuwa wanajihusisha na wizi wa mifugo katika kaunti ya Pokot Magharibu kujihusisha katika kilimo cha maembe na ufugaji wa nyuki baada ya vijana hao kuacha wizi.
Kwa mujibu wa msimamizui wa NRT Tom Lalapaa mpango wa ustahimilivu unaoendezwa na wakfu wa utunzaji wa wanyamapori umebadilisha Maisha ya vijana wengi katika kaunti hiyo na hivyo unapaswa kukumbatiwa na wakaazi wote ili kutokomesha uhalifu.
Naibu gavana wa kaunti ya pokot magharibi Robert Komolle amewataka wahisani kujitokeza kuunga mkono mipango ya aina hiyo ili kuwawezesha vijana kujimudu kimaisha.
Imetayarishwa na Janice Marete