#Local News

KESI INAYOTAKA DIG LAGAT ATIMULIWE YAWASILISHWA

Wakenya kadhaa akiwemo wakili Ndegwa Njiru wamewasilisha kesi mahakamani wakitaka kuondolewa mamlakani kwa naibu inspekta mkuu wa polisi Eliud Lagat kuhusiana na dhuluma alizotendewa bloga Albert Ojwang na kusababisha kifo cha bloga huyo akiwa mikononi mwa maafisa wa polisi.

Kwenye kesi yao, walalamishi wameitaka mahakama kuirodhesha kesi hiyo kuwa ya dharura, huku wakitaka amri itolewe ya kumzuia Lagat kuingia afisini mwake au eneo lolote la idara ya polisi hadi IPOA itakapokamilisha uchunguzi na kesi dhidi ya wahusika kuanza.

Kesi yao imewasilishwa siku moja baada ya kundi la wanaharakati hapo jana kuwasilisha ombi la kutaka kumshtaki Lagat kuhusiana na mauaji hayo.

Imetayrishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *