URENO WATAWAZWA MABINGWA UEFA NATIONS LEAGUE

Cristiano Ronaldo aliiongoza Ureno kuwacharaza majirani zao Uhispania kwenye fainali za kipute cha UEFA Nations League jana usiku, na kuipa ureno taji la pili la fainali za mashindano hayo tangu mwaka wa 2019.
Ronaldo alilazimisha sare ya mabao 2 kunako dakika ya 61 baada ya Uhispania kuchukua uongozi kwenye kipindi cha kwanza kupitia mabao ya Martin Zubimendi na Mikel Oyarzabal
Kwenye matuta ya penalti, Gonzalo Ramos, Vitinha, Bruno Fernandez na Nuno Mendes waliifungia Ureno mikwaju hiyo, ila juhudi za Alvaro Morata ikazuiwa na kipa Diogo Costa, kabla ya Ruben Neves kufunga mkwaju muhimu uliyowatawaza Wareno washindi.
Kabla ya mechi hiyo kuanza, macho yaliangazia mshindi wa Ballon d’or mara 5 Cristiano Ronaldo na kinda wa Uhispania Lamine Yamal, ila wachezaji wengine hasa Oyarzabal yakatamalaki katika jiji la Munich Ujerumani kulikochezewa fainali hizo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa