TSC YALAUMIWA KWA MASAIBU YA WALIMU WA JSS

Tume ya huduma za walimu TSC imelaumiwa kufuatia kutimuliwa kwa baadhi ya walimu wa Shule ya Sekondari ya msingi (JSS).
Haya yanajiri baada ya baadhi ya wabunge wakiongozwa na Seneta wa Nandi Samson Cherargei kutaka tume hiyo ifutilie mbali uamuzi huo la sivyo ikabiliwe bungeni.
Akihutubia wanahabari katika majengo ya Bunge, Cherargei ameitaka TSC ianzishe mchakato wa kuwaajiri walimu zaidi ya 46,000 kwa mikataba ya kudumu.
Cherangei aidha amesema bunge litawaita wasimamizi wa tume hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Nancy Macharia wiki ijayo kueleza uamuzi huo iwapo watashindwa kuubatilisha.
Imetayarishwa na Janice Marete