#Local News

WANDANI WA GACHAGUA WASIKAMATWE, MAHAKAMA

Mahakama kuu imetoa amri ya kuzuia kukamatwa au kuzuiliwa kwa wabunge James Gakuya wa Embakasi Kaskazini na Benjamin Mejja Donk wa Embakasi ya kati wawili hao wakiwa wandamani wa Naibu Rais Rigathi Gachagua kuhusiana na ufadhili wa maandamano ya kupinga uongozi mbaya serikalini.

Wiki jana, wawili hao walikamatwa katika majengo ya bunge na kuhojiwa sawa na wasaidizi watatu wa Gachagua kuhusiana na tuhuma za kufadhili maandamano hayo.

Hata hivyo, jaji Chacha Mwita ametoa agizo hilo baada ya wabunge hao kuwasilisha kesi mahakamani.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *