SAKATA YA MALARIA YAMWANDAMA TUM

Mhandisi Peter Tum aliyeteuliwa na Rais William Ruto kuwa balozi wa Kenya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amelazimika kujitetea dhidi ya sakata ya shilingi bilioni 3.7 za ununuzi wa vyandarua vya kuzuia Malaria alipokuwa katibu mkuu katika wizara ya afya.
Akiwa mbele ya kamati ya masuala ya kigeni katika bunge la kitaifa, Tum amesema uagizaji huo ulifanywa na katibu wa afya ya umma wa wakati huo na wala si yeye.
Miongoni mwa wengine wanaohojiwa ni aliyekuwa waziri wa afya Susan Nakhumicha, aliyeteuliwa kuwa balozi wa Kenya katika shirika la UNHABITAT jijini Nairobi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa