KRA YANYIMWA MPESA, AKAUNTI ZA BENKI ZA WALIPA KODI
Mamlaka ya ukusanyaji Ushuru nchini KRA imepata pigo baada ya ombi lao kutaka kupeleleza akaunti za walipa kodi za Mpesa na benki kukataliwa.
Katika mkakati mpya wa kufichua udanganyifu wa kodi, mtoza ushuru, kupitia Hazina ya Kitaifa, KRA ilitaka kupewa kibali cha kuwa na data za walipa kodi za benki na mpesa.
Mswada wa Fedha, 2024, ulipendekeza kufanyia marekebisho sheria ya ulinzi wa data ili kutoa msamaha wa KRA kutokana na sheria za faragha wakati wa kuchunguza wakwepaji.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































