KOBBIE ATAJWA KWA KIKOSI CHA KWANZA CHA RED DEVILS
Kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo ana furaha kwamba uvumi kuhusu mustakabali wa mkufunzi wa Manchester United Erik ten Hag umeisha, baada ya kupewa nafasi katika kikosi cha kwanza na Mholanzi huyo.
Msimu wa mafanikio wa Mainoo akiwa na hawa Mashetani Wekundu, ambao ulijumuisha kufunga bao la ushindi katika fainali ya Kombe la FA dhidi ya mabingwa wa Uingereza Manchester City, ulimfanya aitwe kwenye kikosi cha Gareth Southgate kwa Euro 2024.
Licha ya kushinda taji la pili katika misimu miwili Old Trafford, mustakabali wa Ten Hag ulisalia mashakani baada ya United kumaliza katika nafasi ya nane kwenye Premier League.
Hata hivyo, Ten Hag alithibitisha Jumapili kuwa ameambiwa na klabu kuwa atasalia kuinoa timu hiyo msimu ujao.
Mainoo aliingia akitokea benchi katika ushindi wa 1-0 wa England dhidi ya Serbia Jumapili na kumfanya kucheza mechi yake ya kwanza ya ushindani katika kikosi cha Southgate.
Uingereza itamenyana na Denmark mjini Frankfurt siku ya Alhamisi na Mainoo anatazamia kukutana na wachezaji wenzake wawili Manchester United, Rasmus Hojlund na Christian Eriksen.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































