WASHUKIWA WA KISUNZI CHA KOIMBURI WAPEWA DHAMANA

Mahakama ya Milimani imewaachia huru washukiwa wanne wanaohusishwa na madai ya utekaji nyara wa mbunge wa Juja George Koimburi kwa dhamana ya shilingi milioni 1 kila mmoja na mdhamini wa kiasi sawa na hicho au bondi ya shilingi elfu 300 pesa taslimu. Hakimu Carolyne Nyaguthii ametoa uamuzi huo amewazuia washtakiwa ambao ni mwakilishi wadi Grace […]

TUMIENI VIVUKO KUEPUSHA MAAFA, POLISI

Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Kikuyu Joseph Ndege, amewataka wakazi kuhakikisha wanatumia vivuko kwenye barabara kuu ya Nairobi kuelekea Nakuru ili kuepusha visa vya ajali anavyosema vimeongezeka kutokana na utepetevu wa wakazi. Wito wake umejiri baada ya dada wawili kugongwa na lori na kufariki papo hapo mapema leo kwenye barabara hiyo karibu nae […]

MADAKTARI WAONYA DHIDI YA VITISHO KIAMBU

Muungano wa madaktari nchini KMPDU umeishutumu serikali ya kaunti ya Kiambu kutokana na vitisho vyake vya kuwafuta kazi madaktari wanaogoma, wakitaja hatua hiyo kuwa kinyume na sheria na ukiukaji wa haki zao. Kwenye kikao na wanahabari, katibu mkuu wa muungano huo Dakta Davji Atellah, ametetea mgomo huo unaoendelea akisema unalindwa kisheria. Madaktari kwenye kaunti hiyo […]

HATUNA MUDA NANYI- WETANG’ULA KWA WAPINZANI

Spika wa Bunge la kitaifa Moses Wetang’ula amewaonya viongozi wanaopinga sera za serikali, akitaja ukosoaji wao kuwa kelele na kwamba haitawazingatia. Akizungumza kwenye hafla ya masomo katika kaunti ya Bungoma, Wetang’ula amewashutumu viongozi wanaopinga kukodishwa kwa kiwanda cha Nzoia, na kusema kuwa wanatumia suala hilo kisiasa. Kauli yake imesisitizwa na gavana wa Bungoma Ken Lusaka […]

JIPU LA MGOMO LATUMBUKA KAKAMEGA

Ni afueni kwa wakazi wa Kakamega baada ya madaktari kwenye kaunti hiyo kusitisha mgomo kufuatia kutia Saini mkataba wa maelewano na serikali ya kaunti hiyo. Kwenye kikao na wanahabari baada ya makubaliano hayo, mkuu wa huduma za afya Dakta Livingstone Imbayi, amesema kuwa watafanya kila wawezalo kuhakikisha makubaliano hayo yanazingatiwa. Imetayarishwa na Antony Nyongesa

SERIKALI MBIONI KUIMARISHA UCHUMI WA BAHARI, MAZIWA

Rais William Ruto ameahidi kuwa serikali yake itaboresha miundomsingi katika sekta ya uchumi unaotegemea raslimali za baharini na maziwani ili kuboresha sekta hiyo na kuongeza mapato. Rais ameyasema haya mjini Homa Bay kwenye kongamano la uchumi wa sekta hiyo, akisema serikali imewekeza shilingi bilioni 4 kwenye sekta hiyo. Rais alikuwa ameandamana na kinara wa ODM […]

MWAKILISHI WADI, WASHTAKIWA WENZA KUJUA HATMA YA DHAMANA

Mwakilishi wa wadi ya Kamyenya-ini kaunti ya Murang’a Grace Wairimu na washtakiwa wenza 3 kwenye kesi inayohusiana na madai ya utekaji nyara wa mbunge wa Juja George Koimburi, watafamu hatma yao ya dhamana majira ya saa nane unusu alasiri hii. Watatu hao wamefikishwa katika mahakama ya Milimani ambapo idara ya DCI imeomba kumzuilia mwakilishi wadi […]

MSASA WA IEBC KUFANYIKA JUMAMOSI

Watu 7 walioteuliwa na Rais William Ruto kuhudumu kama mwenyekiti na makamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC watapigwa msasa hapo kesho na kamati ya sheria na haki katika bunge la kitaifa JLAC, baada ya zoezi hilo awali kuzuiwa na mahakama. Kupitia notisi ya umma iliyochapishwa kwenye magazeti ya humu nchini hii leo, […]

RUTO AWAHAKIKISHIA WAVUVI USALAMA

Wavuvi nchini wamehakikishiwa usalama wa kutosha wanapoendeleza shughuli zao, Rais William Ruto akiahidi kuongeza idadi ya maafisa wa usalama kwenye Ziwa Victoria ili kuwalinda dhidi ya mashambulizi ya mara kwa mara. Ameyasema haya jijini Kisumu, akisema serikali imesaka soko la kimataifa la Samaki ili kuongeza mapato kwenye sekta hiyo Imetayarishwa na Antony Nyongesa

HOFU YA MAFURIKO BUDALANG’I

Wakazi wa Budalang’i kaunti ya Busia wameiomba serikali kuchimba mabwawa makubwa kwenye mito ya Nzoia na Yala ili kudhibiti mafuriko ya kila mara eneo hilo. Wakiongozwa na mbunge wa eneo Raphael Wanjala, wakazi hao wamesema kuwa wameingiwa na hofu ya kusombwa na mafuriko, kutokana na mvua kubwa. Imetayarishwa na Antony Nyongesa