AACHILIWA BAADA YA KUFUNGWA KIMAKOSA MIAKA 13
Shangwe na nderemo zilijaa nyumbani kwa Peter Githinji Kioi, mkazi wa kijiji cha Kiangothe Kirinyaga ya Kati, aliporejea nyumbani baada ya kukaa gerezani kwa miaka 13.
Githinji, ambaye alikuwa akitumikia kifungo cha maisha jela katika Magereza ya King’ong’o, aliachiliwa baada ya kufanikiwa kukata rufaa dhidi ya hukumu yake.
Masaibu ya Githinji yalianza mkewe alipomshtumu kwa kumnajisi binti yao, shtaka lililopelekea kifungo chake cha awali cha miaka 20.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































