KAUNTI ZAHIMIZWA KUWASILISHA PENSHENI YA WAFANYAKAZI
Katika juhudi za kuwaepushia mahangaiko wafanyakazi wa kaunti wanaostaafu, serikali za kaunti zimehimizwa kuwasilisha malipo ya pensheni kwa hazina ya pensheni ya serikali ili kuwawezesha wafanyakazi hao kujitegemea baada ya kustaafu.
Akizungumza kwenye mkutano wa kitaifa wa hazina hiyo, katibu wa muungano wa wafanyakazi wa kaunti Roba Duba, amesema hadi sasa muungano huo unazidai kaunti zaidi ya shilingi bilioni 30.
Kauli yake ikungwa mkono na naibu msimamizi wa hazina ya pensheni ya kaunti Joseph Rono.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































