MENEJA WA UWEKEZAJI KUJUA HATIMA YAKE LEO

Jaji wa Mahakama ya Juu Nixon Sifuna leo hii anatarajiwa kutoa uamuzi wake katika rufaa iliyowasilishwa na aliyekuwa meneja wa uwekezaji Francis Moturi baada ya kupatikana na hatia katika kesi inayomkabili ya kusababisha hasara ya shilingi bilioni 1.2 katika wizara ya NSSF.
Mahakama ya Hakimu Mkazi ilimpata na hatia mnamo Januari 2022 na kumhukumu kifungo cha miaka 14 jela au kulipa faini ya Shilingi bilioni 2.6 ili kuachiliwa.
Imetayarishwa na Janice Marete