KAUNTI YA KISUMU IMESITISHA MCHAKATO WA KUWAAJIRI WAHUDUMU WAPYA WA AFYA

Serikali ya kaunti ya Kisumu imesitisha mpango iliokuwa nao wa kuwaajiri wahudumu wa afya wakiwemo madaktari kwa kandarasi.
Mwenyekiti wa chama cha madaktari KMPDU Dennis Miskela amesema kuwa amezungumza na gavana wa Kisumu Anyang Nyongo ambaye amesema hatua hiyo inafuatia kusitishwa kwa mgomo wa madaktari
Kaunti ya Kisumu ilikuwa imetangaza nafasi za mafiasa wa afya ambao wangeajiriwa kwa kandarasi ya miezi 6.
Kwa mujibu wa Miskela kaunti ya Kisumu ililenga kuwaajiri maafisa hao iwapo mgomo ungeendelea.