ELITE YABADILIKA KUA UNITED
Sasa ni rasmi timu ya Mombasa Elite inayoshiriki ligi ya NSL imebadili jina na sasa itakuwa inajulikana kama Mombasa United.
Kulingana na meneja mkuu wa timu hii Fedinad Ogot anasema hili limeafikiwa baada ya kujitokeza kwa mfadhili mpya na ambaye amejitolea kuisaidia timu hiyo.
Kwa sasa Mombasa United wameanza mazoezi huku wakiwa mbioni kupata sajili mpya za kupambana msimu mpya wa 2024- 2025.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































