USAID: WAFANYAKAZI KAJIADO KUPEWA AJIRA MPYA

Wafanyakazi waliokuwa wakihudumu chini ya ufadhili wa shirika la USAID kwenye kaunti ya Kajiado wamepata afueni baada ya serikali ya kaunti hiyo kuwahakikishia kuwa watahamishiwa katika idara nyingine baada ya ajira yao ya shirika hilo kukatizwa.
Akizungumza katika eneo la Kajiado ya kati, gavana wa kaunti hiyo Joseph Ole Lenku amewahimiza magavana wenzake kuiga mfano huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa