DPP INGONGA NDIYE RAIS WA APA
Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Renson Ingonga amechanguliwa kwa kauli moja kuwa rais wa chama cha wakurugenzi wa mashtaka barani afrika APA, na kuchukua mahali pa mwanzake Mohammed Sawqi Ayyad wa Misri.
Uchaguzi wake umefanyika wakati wa kongamano la 17 la kila mwaka lilioandaliwa jijini Marrakech, Moroko.
Katika hotuba yake ya kukubali uchaguzi huo, Ingonga ameahidi kujitolea kwake kufanikisha malengo ya chama hicho.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































