LIVERPOOL KARIBU KUTWAA UBINGWA LICHA YA WIKI NGUMU

Liverpool wapo karibu kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza, lakini hali ya sintofahamu imetanda baada ya wiki ngumu.
Walipoteza fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya Newcastle, siku chache baada ya kutolewa na PSG kwenye Ligi ya Mabingwa. Newcastle walitawala mchezo na kushinda taji lao la kwanza baada ya miaka 70.
Hata hivyo, Slot ameelekeza mawazo kwa Ligi Kuu ambapo Liverpool wanaongoza kwa alama 12, wakihitaji pointi 16 zaidi ili kutwaa taji, hata kama Arsenal watashinda mechi zao zote.
Imetayarishwa na Janice Marete