NCIC; RIPOTI KESI ZA UCHOCHEZI
Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano NCIC inachunguza visa 43 vya matamshi ya chuki yaliyoripotiwa kati ya Aprili na Juni mwaka huu huku ikilenga kuhimiza kuwepo kwa amani nchini.
Katika taarifa yake tume hiyo imesema kesi hizo ziko katika hatua mbalimbali za uchunguzi na kwamba ni sehemu ya ripoti 67 ambazo zimeripotiwa.
NCIC pia imehimiza umma kuripoti kesi zinazoweza kuchochea hisia za dharau, chuki, ghasia, ubaguzi na pia zile zinazoweza kuathiri amani nchini kupitia Huduma ya Ujumbe Mfupi (SMS) nambari 1547 bila malipo.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































