MTOTO, 3, AFARIKI BAADA YA KULA NYOKA

Familia moja katika eneo la kavuvuani eneo la MWingi West kaunti ya Kitui inaomboleza kifo cha mwanao mwenye umri wa miaka 3 aliyefariki baada ya kula mabaki ya nyoka aina ya Black Mamba.
Nyoka huyo aliyekuwa ameuawa na nyanyake mtoto huyo alikuwa amewekwa jikoni akisburi kuchomwa.
Naibu Chifu eneo hilo Eunice Mulwa amelalamikia wingi wa nyoka eneo hilo na kuwataka maafisa wa KWS kuwakusanya.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa