RUTO AKOSOA VYUO, AAMURU BARUA MPYA ZIANDIKWE

Rais William Ruto sasa anasema kwamba kiwango cha karo kilichokuwa kimeorodheshwa kwenye barua za vyuo vikuu kuwaalika wanafunzi wapya kilikuwa na dosari, akisema kiwango hicho ni gharama ya kipindi kizima cha kusomea kozi husika na wala si mwaka mmoja.
Akizungumza kwenye eneo la Ogembo kaunti ya Kisii, Rais amesema kwamba serikali itaviamuru vyuo hivyo kuandika upya barua mara moja ili kuondoa kasoro hizo.
Aidha, Ruto amekariri kwamba serikali imebadili mfumo wa utoaji wa ufadhili wa elimu ya vyuo vikuu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa