KNCCI WAPINGA MSWADA WA BAJETI 2024-2025

Chama cha wafanyibiashara nchini KNCCI kimepinga adhabu baina ya shilingi milioni 2 kwa biashara ambazo zitakiuka agizo la kulipa kodi kutumia mfumo wa kieletronik maarufu Etims.
Katika taarifa kwa vyombo vya Habari rais wa KNCCI Erick Rutto amekosoa mswada wa mwaka wa kifedha wa 2024 unaopendekeza biashara kulipa kiwango hicho chja fedha kwa kukosa kutumia etims.
Rutto amesema adhabu hiyo ni kali na huenda ikachan gia kudorora kwa biashara ndogo ndogo kwa ngingi zao hazijafahamu vyema matumizi ya etims.
KNCCI aidha inataka serikali kuwekeza Zaidi katika kuwahamasisha wamiliki wa biashara ndogo ndogo jinsi ya kutumia mfumo huo badala ya kuwachukulia hatua wasiofanya hivyo.
Imetayarishwa na: Janice Marete
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































