WABUNGE WATISHIA KUMBANDUA MURKOMEN
Wabunge wanaogemea mrengo wa aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua wametishia kuwasilisha bungeni hoja ya kumtimua kutoka mamlakani waziri wa usalama Kipchumba Murkomen kutokana na amri yake inayowataka polisi kuwafeytulia risasi wanaokaribia vituo vya polisi.
Wakiongozwa na mbunge wa Manyatta kaunti ya Embu Gitonga Mukunji, wabunge hao wamesema amri hiyo inalenga kuendeleza mauaji ya kiholela.
Hata hivyo, Mukunji amehofia hoja hiyo kukosa kufanikiwa kwa madai kwamba bunge limetekwa na serikali tendaji.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































