EMERGING STARS WACHARAZA ZIMBABWE 2-0

Emerging stars jana walirejea katika njia za ushindi katika michuano ya Cosafa mwaka huu inayoendelea ambapo waliandikisha ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Zimbabwe katika uwanja wa Wolfson mjini port Victoria Afrika Kusini
Osteen Odhiambo alifunga mbao la kwanza dakika ya 54 naye benson Omala akaongeza la pili dakika ya 73.
Emerging starrs walimaliza katika nafasi ya pili katika kundi la B ikiwa na point 6 sawa na walio kileleni Komoro itajua iwapo itafuzu kwa nuru fainali kama mojawapo ya washindi wa pili bora baada ya mechi za kundi C kukamilika hii leo
Kocha mkuu wa Emerging Stars Ken Odhiambo amemsifia timu hiyo baada ya kupata ushindi muhimu ili kuendeleza matarajio yao ya kuwania taji la Cosafa mwaka huu
Imetayarishwa na Janice Marete