#Business

ADA ‘DHALIMU’ ZAWAFUKUZA WAWEKEZAJI- KNCCI

Rais wa Chama cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda nchini Kenya (KNCCI), Dkt. Erick Rutto, amekosoa ongezeko la ada na masharti mengi yanayowakabili wajasiriamali wanapotaka kuanzisha biashara, akisema hali hii inakatisha tamaa wawekezaji na kuathiri mazingira ya biashara nchini.

Akitolea mfano wa kampuni moja ya upakiaji wa chakula inayopanga kuanzisha shughuli zake katika Kaunti ya Kajiado, Dkt. Rutto amesema kampuni hiyo inahitajika kulipia zaidi ya vibali 20 vinavyogharimu jumla ya shilingi 337,000.

Dkt. Rutto anapendekeza kuwepo kwa mpango wa kulipa ushuru kwa awamu, ikiwa ni pamoja na likizo ya hadi miaka miwili kwa kampuni mpya, hatua anayosema itawezesha biashara kustawi na baadaye kuchangia kikamilifu katika upanuzi wa wigo wa walipakodi nchini.

Imetayarishwa na Mercy Asami

ADA ‘DHALIMU’ ZAWAFUKUZA WAWEKEZAJI- KNCCI

SERIKALI YAKARIRI SHARTI ILIPWE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *