MAWAZIRI WA KILIFI WATAKIWA KUKAMILISHA MIRADI ILIYOKWAMA

Mwakilishi wa wadi ya Adu eneoi bunge la magarini kaunti ya Kilifi Samson Zia amewalaimu mawaziri wa kaunti hiyo kwa kukosa kutekeleza miradi ya serikali iliyopita katika maendeo mbali mbali ya kaunti ya Kilifi.
Kwa mujibu wa Zia miradi nyingi ya maendeleo mashinani imekwama kwa muda mrefu sasa tangu serikali ya aliyekuwa gavana wa kaunti hiyo Amason Jefa Kingi kuondoka mamlakani huku akiwahimiza mawaziri na viongozi wenzake kuhakikisha miradi iliyokwama inatekelezwa.
Imetayarishwa na Janice Marete