PVK YAITAKA SERIKALI KUWAJIBIKIA WAKENYA

Viongozi wa kidini wa Pentecostal Voice Of Kenya wamejitokeza kukashifu machafuko ya kisiasa yanaoendele humu nchini haswa suwala la kubanduliwa mamlakani kwa naibu wa rais Rigathi Gachagua
Wakiongozwa na mwenyekiti wao Apostal Peter Manyuru ambaye pia ni mwazilishi wa kanisa la Jesus Teaching Ministry JTM wamesema kuwa huenda serikali ina njama ya kuwafumba macho wananchi wasifuatilie maswala muhimu yanalikabuili taifa hili haswa swala la kampuni ya adani kuchukua usukani katika usimamizi wa uwanja wa kimataifa wa ndege JKIA
Aidha wameitaka serikali kutekeleza ahadi zake kwa wananchi nkwa kuboresha uchumi jinsi walivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2022
Imetayarishwa na Janice Marete