#Local News

MWAKILISHI WADI, WASHTAKIWA WENZA KUJUA HATMA YA DHAMANA

Mwakilishi wa wadi ya Kamyenya-ini kaunti ya Murang’a Grace Wairimu na washtakiwa wenza 3 kwenye kesi inayohusiana na madai ya utekaji nyara wa mbunge wa Juja George Koimburi, watafamu hatma yao ya dhamana majira ya saa nane unusu alasiri hii.

Watatu hao wamefikishwa katika mahakama ya Milimani ambapo idara ya DCI imeomba kumzuilia mwakilishi wadi huyo kwa siku 14, na siku 15 kwa wenzake ili kukamilisha uchunguzi kwenye tukio hilo.

Hata hivyo, mawakili wa washtakiwa wamepinga ombi hilo wakitaka waachiwe huru kwa dhamana.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MWAKILISHI WADI, WASHTAKIWA WENZA KUJUA HATMA YA DHAMANA

MSASA WA IEBC KUFANYIKA JUMAMOSI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *