POLISI WAWILI WAKAMATWA KIRINYAGA
Maafisa wawili wamekamatwa kwa madai ya kushirikiana na mshukiwa wa mauaji raia wa Uganda katika kaunti ya Kirinyaga.
Mshukiwa huyo anayedaiwa kutoroka katika kituo cha polisi cha Kiamasiri alikamatwa mwezi uliopita kwa tuhuma za mauaji ya mwajiri wake novemba mwaka jana.
Kwa mujibu wa familia ya marehemu mshukiwa alitoroka ijumaa wiki iliyopita kabla ya kufikishwa mahakamani leo hii.
Imetayarishwa na Janice Marete.
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































