MGOMO WAFUTILIWA MBALI MACHAKOS
Ni afueni kwa wakaazi wa Machakos baada ya maafisa wa kliniki kufutilia mbali mgomo wao uliopangwa kuanza usiku wa leo.
Hii ni baada ya maafisa wa muungano wa wahudumu hao kutia Saini mkataba wa maelewano na serikali ya kaunti ya Mchakos ukilenga kuangazia lalama walizoibua.
Kupitia mwenyekiti wao wa kitaifa Peterson Wachira wanasema miongoni mwa masuala hayo ni kupandishwa vyeo kwa maafisa ambao wamesalia katika kiwango kimoja kwa muda na kuongezwa kwa mshahara.
Imetayarishwa na Maureen Mukhobe
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































