JAJI MUSTAAFU MUTUNGA NA KARUA WASHTAKI TANZANIA
Kuna haja ya wapatanishi kuingilia kati na kuondoa uhasama uliopo kati ya wanaharakati wa humu nchini na serikali ya tanzania.
Hii ni baada ya aliyekuwa jaji mkuu Willy Mutunga na mwanasiasa Martha Karua kuwasilisha kesi Katika mahakama ya haki ya afrika mashariki dhidi ya serikali hiyo kwa kosa la kuwazuilia kinyume na sheria na kuwazuia kuingia nchini humo.
Wanaharakati hao wakiwa pamoja na wengine Gloria Kimani Lynna Ngugi Hussein Khalid na Hanisa Adan wanataka msamaha kutoka kwa serikali ya Tanzania.
Imetayarishwa na Maureen Amakhobe
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































