#Local News

WAFANYAKAZI WA MRADI WA NYUMBA WAGOMA BUSIA

Shughuli za ujenzi katika mradi wa serikali wa makazi ya bei nafuu katika eneo la Alema, eneo bunge la Funyula kaunti ya Busia zimekwama baada ya wafanyakazi kwenye mradi huo kugoma, wakimlaumu msimamizi kwa madai ya kutowasilisha matozo yao ya bima ya SHA na NSSF kwa afisi husika.

Wakizungumza na wanahabari baada ya kususia kazi, wafanyakazi hao aidha wamelalamikia malipo duni mbali na kufanya kazi kwa muda wa saa 9 badala ya 8 inavyostahili.

Wamemtaka msimamizi huyo kuhakikisha malalamishi yao yanaangaziwa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

WAFANYAKAZI WA MRADI WA NYUMBA WAGOMA BUSIA

ABAUTANI YA WAFUGAJI KAJIADO KUHUSU CHANJO

WAFANYAKAZI WA MRADI WA NYUMBA WAGOMA BUSIA

SUSWA: IPOA YAAHIDI HAKI KWA WAATHIRIWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *