BAJETI YAFANYIWA MAREKEBISHO KUPUNGUZA NAKISI
Katika juhudi za kupunguza nakisi ya bajeti, Baraza la Mawaziri limeazimia kutekeleza marekebisho muhimu ya bajeti, kwa mujibu wa sera ya serikali ya ujumuishaji wa fedha.
Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika mjini Nairobi na kuongozwa na Rais William Ruto kiliagiza mawaziri kushirikiana na Hazina ya Kitaifa kutambua na kutekeleza marekebisho yanayohitajika katika wizara zao na idara za serikali.
Taarifa imesema kwamba marekebisho haya ni sehemu ya hatua za kupunguza matumizi, kuboresha nidhamu ya fedha, na kupunguza hatari ya deni la umma, ili kuunda mazingira bora ya kifedha kwa ajili ya kutoa huduma muhimu kwa wananchi.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































