DEMBELE ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA LIGUE 1 BAADA YA KUIBUKA KINARA PSG
Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Ousmane Dembele ametajwa kuwa mchezaji bora wa Ligue 1 msimu huu, baada ya kuiongoza PSG kutwaa taji lao la 13 la Ufaransa na kufuzu fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Dembele ndiye kinara wa mabao msimu huu akiwa na mabao 21 katika Ligue 1, na jumla ya mabao 33 katika mashindano yote, ikiwemo mabao manane barani Ulaya.
Anachukua nafasi ya Kylian Mbappe aliyeshinda tuzo hiyo mara tano mfululizo kabla ya kujiunga na Real Madrid mwishoni mwa msimu uliopita. Kocha wa PSG, Luis Enrique, alituzwa kocha bora wa msimu katika hafla ya tuzo za UNFP (muungano wa wachezaji wa Ufaransa), huku Desire Doue akinyakua tuzo ya mchezaji chipukizi bora.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































