#Local News

KMPDU YAGAWANYIKA?

Huku madaktari wakianza mgomo wao wa kushinikiza kuajiriwa kwa wenzao wanagenzi, dalili za mgawanyiko zimeanza kuchipuka katika uongozi wa muungano wao wa kitaifa KMPDU.

Katika maandamano ya kutaka kupiga kambi nje ya makao makuu ya wizara ya Afya, madaktari hao wameimba wimbo wa kumkashifu naibu katibu mkuu wa KMPDU Dennis Miskellah ambaye hawana imani naye.

Mapema leo, akaunti ya X ya muungano huo ilichapisha ujumbe ikisema mgomo umefutiliwa mbali, kabla ya ujumbe huo kufutwa na kisha katika mkuu Davji Atella akidai kwamba akaunti hiyo ilikuwa imedukuliwa.

Hata hivyo, madaktari hao wanaendelea kumiminika n je ya afisi za Afya House jijini Nairobi wakitaka madaktari wanagenzi kuajiriwa kwa awamu moja.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KMPDU YAGAWANYIKA?

NIKO SALAMA;SYLVANUS OSORO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *