SAKAJA AAMURU UKAGUZI MPYA WA MIRADI

Gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja amebuni jopokazi kwa jukumu la kukagua upya miradi ya ujenzi iliyoidhinishwa kwa muda wa miaka miwili iliyopita, hatua inayolenga kuhakikisha kuwa miradi au majengo hayo yanakidhi viwango vilivyowekwa.
Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, Sakaja amesema tayari serikali ya Kaunti ya Jiji hilo kupitia ofisi ya kaimu Katibu wa Kaunti imewaandikia wadau husika na kuwataka kuwasilisha majina ya wataalamu na wawakilishi ambao watakuwa sehemu ya jopokazi hilo
Amesema wamajopo hao watakutana tarehe 12 mwezi huu ili kuanza ukaguzi huo, na wamepewa siku 60 za kukamilisha kazi hiyo na kuwasilisha ripoti kwa ajili ya utekelezaji.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi