CHIDZUGA AOMBA WANAWAKE WAFANYWE KIPAUMBELE KWENYE AJIRA

Naibu msemaji wa serikali Mwanaisha Chidzuga ametoa wito kwa sekta mbali mbali za uajiri nchini kuwapa kipaumbele wanawake katika utoaji wa nafasi za ajira.
Akizungumza jijini Mombasa wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake walioko katika sekta ya bahari, Chidzuga amesema hatua hiyo itahakikisha azma ya kuwapa wanawake nafasi sawa za uongozi na wanaume.
Kauli yake imeisistizwa na mwenyekiti wa chama cha wanawake katika sekta ya bahari tawe la Kenya Winnie Maina.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa