KAUNTI YA NAIROBI YAORODHESHA MALI KWA MNADA

Serikali ya kaunti ya Nairobi imetishia kuvipiga mnada vipande vya ardhi katikati ya jiji kwa madai ya kukosa kulipia ada za arthi nchini.
Katika notisi ya kurasa 72 iliyochapishwa leo Ijumaa, Gavana Johnson Sakaja ameonya kuwa kushindwa kulipa viwango vya ardhi kutasababisha kupigwa mnada kwa sehemu husika za ardhi.
Sehemu ya arthi iliyoorotheshwea katika notisi hiyo inapatikana katika maeneo bunge ya Westlands , Starehe, Ruaraka, Roysambu Mathare, Makandara Langata, Kasarani Kibra Embakasi Magharibi , Embakasi mashariki, Dagoreti kusini na Dagoreti kaskazini.
Imetayarishwa na: Janice Marete