MAHAKAMA YAHARAMISHA KARO YA ZIADA

Mahakama imewapa afueni wazazi kwa kurahamisha hatua za shule za umma kuwatoza ada za ziada bila idhini ya wizara ya elimu nchini.
Uamuzi huo wa mahakama unafuatia kesi iliyowasilishwa dhidi ya shule ya upili ya St. Georges iliyowataka wazazi kulipa ada za ziada, mahakama ikisema hatua hiyo na haramu.
Kwenye kesi hiyo, mahakama ilibaini kuwa shule hiyo iliwataka wazazi kugharamia masuala kadhaa ikiwemo ujenzi wa bweni na kufadhili mapungufu ya fedha kwenye bajeti ya shule.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa