#Football #Sports

POLICE BULLETS WAFYTUA USHINDI

Hapo jana Wawakilishi wa Kenya kwenye mashindano ya kufuzu kwa makala ya nne ya ligi klabu bingwa barani Afrika ukanda wa Cecafa, Kenya Police Bullets walipata ushindi wao wa kwanza kwa kuilaza Rayon Sports Women ya Rwanda 1-0 kwenye mechi yao ya pili ya kundi A, iliyosakatwa katika uwnaja wa Abebe Bikila jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Puren Alukwe ndiye aliyefunga bao hilo la pekee dakika ya saba ya mchezo na hivyo kuwaweka maafande hao kwenye nafasi bora ya kufuzu nusu fainali kwani wanahitaji alama moja pekee kwenye mechi yao ya mwisho ya makundi dhidi ya CBE ya Ethiopia Alhamisi hii.

Ushindi huo ulikuwa muhimu kwa Police kufuatia sare tasa dhidi ya Yei Joint Stars ya sudan Kusini Jumamosi iliyopita.

Kwengineko wenyeji CBE imeibuka timu ya kwanza kufuzu nusu fainali baada ya kuwangusha Yei Joint Stars 4-0 , ushindi ulifuatia ule wa 3-2 dhidi ya Rayon Sports.

Chris Oguso ni afisa mkuu wa Police ambaye kando na kuwapongeza akina dada wake, ameeleza imani ya kufuzu nusu fainali Alhamisi.

Imetayarishwa na Nelson Andati

POLICE BULLETS WAFYTUA USHINDI

NYOTA YA MADINA YAREJESHWA

POLICE BULLETS WAFYTUA USHINDI

VIONGOZI WA ODM KAKAMEGA WAMFOKEA JUSTUS KIZITO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *