TIMU YA SHABANA WAMEBORESHA MUUNDO WA BASI LAO BAADA YA MALALAMIKO KWA WACHEZAJI
Klabu ya soka ya ligi kuu nchini FKL-PL, Shabana fc, wameboresha muundo wa basi lao huku wiki ya pili ya mechi ya ligi msimu huu zikitarajiwa kuendelea.
Kupitia ukurasa wao wa x, maarufu twitter, Shabana FCwaliamua kufanyia basi la timu mabadiliko ili kuwapa wachezaji starehe wanaposafiri kote nchini kwa ajili ya mechi za FKF.
Haya ni mojawapo ya mbinu ambazo timu hiyo inazingatia kuweka maslahi ya wachezaji mbele.
Idadi ya viti vya basi hilo vimepunguzwa kutoka 52 hadi 36 ili kufanya usafiri kuwa wa starehe zaidi bila wachezaji kufinyana.
Shabana FC ilirejea kwenye ligi baada ya muda wa miaka 17.
Imetayarishwa na Kennedy Osoro
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































