WAKULIMA MACHAKOS WAPATA ‘MBEGU ZA MATUMAINI’
Wakulima katika kaunti ya Machakos wamepata afueni baada ya serikali ya kaunti hiyo kuzindua mpango wa kuwapa mbegu za kupanda msimu huu wa mvua ya vuli.
Akizindua mpango huo katika eneo la Matuu, gavana Wavinya Ndeti amesema kuwa wanalenga wakazi walio na mapato ya chini kwa lengo la kuimarisha utoshelevu wa chakula.
Mbegu za mahindi, maharagwe na nyasi za mifugo zimeanza kusambazwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































