HATUFADHILI MAANDAMANO

Mashirika mbali mbali katika kaunti ya Transnzoia yamepinga madai yaliyoibuliwa kwamba mashirika ya kutetea haki za binadamu yamekuwa yakifathili maandamano ya vijana kupitia fedha wanazopokea kutoka kwa wakfu wa Ford Foundation.
Mashirika hayo yamesema kuwa serikali inapaswa kutilia maanani malalamishi yaliyoibuliwa na vijana wa humu nchini badala ya kuyalaumu mashirika hayo.
Imetayarishwa na Janice Marete