#Local News

WATU 7 WAKAMATWA ELDORET KWA KUHUSISHWA NA ULAGHAI

Polisi mjini Eldoret wamewatia mbaroni washukiwa saba wanaohusishwa na ulaghai ya kuajiri watu wanaotafuta ajira nje ya nchi katika eneo hilo.

Kamanda wa polisi wa Kaunti ya Uasin Gishu Benjamin Mwanthi amesema washukiwa hao walikamatwa katika afisi kadhaa ambapo wanahudumu ndani ya mji huo.

Timu za usalama bado zinaendeleza msako mkali ili kuwakamata washukiwa zaidi wanaohusika na njama hizo.

Wakazi wa mkoa huo wanadaiwa kupoteza zaidi ya Shilingi bilioni 10 kutokana na elimu ya nje ya nchi na ulaghai wa ajira kutoka nje ya nchi.

Wakati wa msako huo, maafisa wa upelelezi DCI wamepata watu wengi waliokuwa wakitafuta kazi ambao walikuwa bado wamejipanga katika baadhi ya afisi za maajenti walaghai.

Imetayarishwa na Janice Marete

WATU 7 WAKAMATWA ELDORET KWA KUHUSISHWA NA ULAGHAI

KUPPET YASAMBARATISHA MASOMO BUNGOMA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *