#Local News

MWANGAZA KUCHUNGUZWA NA SENETI NZIMA

Maseneta wameamuru kwamba watasikiliza kwa Pamoja hoja ya kumbandua gavana wa Meru Kawira Mwangaza baada yao kupinga pendekezo la kutaka kubuniwa kwa kamati yenye wanachama 11 kusikiliza hoja hiyo.

Hoja hiyo imewasilishwa bungeni na kiranja wa walio wengi ambaye pia ni seneta wa Kakamega Boni Khalwale, huku Spika Amason Kingi akipendekeza kubuniwa kwa kamati hiyo.

Maseneta waliokuwa wamepndekezwa kusikiliza hoja hiyo ni Hillary Sigei, Abdul Haji, Wahome Wamainga, David Wafula, Gloria Orwoba, Karen Nyamu, Issa Juma, Eddy Oketch, Shakilla Abdalla, Betty Montet na Beatrice Akinyi.

Wakati uo huo, Kingi amewapa wahusika kwenye kesi hiyo hadi Jumamosi hii kuwasilisha hoja zao kwa karani wa bunge hilo, huku vikao vya kusikiliza hoja hiyo vikiratibiwa Jumattatu na Jumanne wiki ijayo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MWANGAZA KUCHUNGUZWA NA SENETI NZIMA

MUDAVADI AISHUKURU UAE KWA KUTOA NAFASI ZA

MWANGAZA KUCHUNGUZWA NA SENETI NZIMA

HAKUNA KUFICHA SURA, MAHAKAMA YAAMURU POLISI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *