#Football #Sports

SIKU YA KENYA POLICE FC

Maelfu ya wapenzi wa soka wanatarajiwa kumiminika katika Uwanja wa Police DT siku ya Jumamosi kwa ajili ya Sikukuu ya Kenya Police FC inayosubiriwa kwa hamu.

Hafla hiyo itaanza saa 10 a.m. hadi 5 p.m, kwa msururu wa shughuli za kusisimua, ikiwa ni pamoja na mechi inayotarajiwa kwa hamu kati ya Kenya Police FC na Shabana FC saa tisa alasiri huku wenzao wa kike.

Police Bullets wakimenyana na Mathare Women FC katika pambano la saa sita mchana.

Kivutio kikuu cha hafla hiyo kitakuwa kuzinduliwa kwa wachezaji wapya waliosajiliwa na Kenya Police FC kabla ya msimu mpya.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Kenya Police FC Carol Kiambi alisisitiza umuhimu wa siku hiyo, akiangazia kujitolea kwa klabu katika uwezeshaji wa jamii na kusherehekea mafanikio yao.

Imetayarishwa na Nelson Andati

SIKU YA KENYA POLICE FC

ILINIVUNJA MOYO SANA

SIKU YA KENYA POLICE FC

AMEENDA MBELE ZA HAKI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *