KIFUNGO CHA MIAKA 20 JELA KWA MWANAMKE ALIYEMUUA MUMEWE

Liza Koima, mwanamke anayedaiwa kumuua mumewe katika ugomvi wa kinyumbani miaka 4 iliyopita amefungwa miaka 20 jela.
Akitoa uamuzi huo, Jaji wa Mahakama Kuu ya Eldoret, Reuben Nyakundi ametaja kosa hilo kuwa kubwa.
Hakimu Nyakundi amebainisha katika hukumu yake kuwa hata baada ya kutenda kosa hilo, mshtakiwa hakuona vyema kuwasiliana na familia ya marehemu Abraham Lagat kuomba msamaha.
Mfanyabiashara huyo aliyeuawa mnamo Agosti 27, 2020, nyumbani kwake eneo la Kipkorgot.
Koima alikamatwa na maafisa wa polisi kama mshukiwa mkuu.
Imetayrishwa na Janice Marete