ODINGA ATOA ARDHI KWA SERIKALI
Mpango wa serikali kujenga makazi ya bei nafuu kwa wakazi wa Kisumu umepigwa jeki, baada ya kinara wa ODM Raila Odinga kutoa hisani ya ekari 5 za shamba la kifamilia katika eneo la Kirembe ili kufanikisha ujenzi wa nyumba hizo.
Akiwa kwenye ziara yake, Rais Ruto amempongeza Odinga kutokana na hisani hiyo, akisema serikali itawekeza shilingi bilioni 3.5 kuwezesha ujenzi huo utakaowanufaisha takribani wakazi 1,000.
Naye Odinga amesema makazi hayo yatasaidia kupunguza matatizo ya nyumba eneo hilo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































