LIPO TUMAINI HAITI, RAIS RUTO
Rais William Ruto ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuzidisha juhudi za kurejesha utulivu nchini Haiti, akikariri haja ya kuimarisha usalama na Maisha ya raia wa taifa hilo la Karibia.
Akizungumza katika kongamano la viongozi kujadili mustakabali wa Haiti, Ruto amehimiza jamii hiyo kuisaidia Haiti kurejesha hali ya utulivu nchini humo.
Aidha, Ruto ambaye maajuzi amtembelea taifa hilo, ameonyesha matumaini kuhusiana na hali ya kawaida kurejelewa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































