#Local News

MAAFISA WA KLINIKI WAILAUMU SERIKALI KWA KUEPUKA MASUALA YAO WAKATI MGOMO WA KITAIFA UKIENDELEA

Shirikisho la Maafisa wa Kliniki la Kenya (KUCO) limelaani serikali kwa kutumia nguvu kupita kiasi huku mgomo wao ukiendelea.

KUCO inadai serikali imeshindwa kushughulikia masuala yao, kama vile ubaguzi wa Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA) na kukataa kutoa nafasi kwa vituo vya afya vinavyomilikiwa na maafisa wa kliniki.

Maafisa wa kliniki wametoa notisi ya mgomo wa siku 14 kutokana na kuzuiwa kutoka kwa SHA na uvunjaji wa makubaliano ya kurudi kazini ya mwaka jana.

Aidha wanadai kutambuliwa mara moja na kuingizwa kwenye orodha ya watoa huduma za afya, na utekelezaji wa makubaliano ya kurudi kazini ifikapo Januari 19, la sivyo watasitisha huduma zao

Imetayarishwa na Janice Marete

MAAFISA WA KLINIKI WAILAUMU SERIKALI KWA KUEPUKA MASUALA YAO WAKATI MGOMO WA KITAIFA UKIENDELEA

CITY YARUDI KATIKA KIWANGO BORA BAADA YA USHINDI

MAAFISA WA KLINIKI WAILAUMU SERIKALI KWA KUEPUKA MASUALA YAO WAKATI MGOMO WA KITAIFA UKIENDELEA

WATU WATANO WAFARIKI KATIKA AJALI HUKO MIGORI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *